JINSI YA KUSAJIRI BLOGU TCRA
Kwa wenye ndoto za kusajili Blog zao nchini Tanzania kama sheria inavyotaka wanapaswa kupitia njia zifuatazo.
1. Kusajili Kampuni Brela (Inachukua siku 1-2 kama una viambata vyote vinavyohitajika kama Jina la kampuni tarajiwa, Kitambulisho cha taifa, tin 2 za ma director, ada ya usajili (hutofautiana kulingana na size ya kampuni), Memorandum na basic information (unaweza kujisajili online)
2. Baada ya kusajiliwa Brela unapaswa kwenda TRA kupata TIN ya kampuni pamoja na Tax clearance utakayopewa mara baada ya kulipa kodi na stamp duty.
3. Unatembelea website ya TCRA na unakwenda sehemu ya Online Content Application System (upande wa kulia juu kama unatumia pc)
4. Unaingiza taarifa zako na ku attach kopi ya documents zifuatazo ambazo ni lazima zithibitishwe na wakili 1. Cheti cha usajili wa kampuni toka Brela, Tax clearance uliyopewa TRA, CV ya atakaye/watakaohusika ktk kuendesha blog yako, Risiti ya malipo ya laki 1 unayopaswa kulipia ktk account ya TCRA kama ada ya maombi na link ya blog yako (URL).
5. Baada ya kupita njia hizo utasubmit mbi lako TCRA nao watahakiki taarifa zako na kuichunguza blog uliyowasilisha kama ina stahili au la
6. kama ina stahili watakujulisha kupitia mfumo na nakala ktk barua pepe yako kuwa unatakiwa kulipa MILIONI 1 kwaajili ya leseni na unatakiwa kulipa kupitia account za TCRA za NBC na NMB
7. Baada ya kulipa unarejea kwenye mfumo na ku attach risiti ya malipo na kui submit kwao
8. Leseni itaandaliwa na utaifuata.
9. Sasa utaruhusiwa kuanza shughuli zako
10. Pitia vyema sheria kabla ya kuanza kuporomosha post kwenye blog yako usije ukapata kipigo cha MBWA KOKO
0 Maoni